Home Burudani Bieber, Baldwin mahaba niue

Bieber, Baldwin mahaba niue

1532
0
SHARE

NEW YORK, Marekani

MWANAMUZIKI Justin Bieber, amekuwa kwenye dimbwi zito la mahaba na mpenzi wake mpya, Hailey Baldwin, ambaye anatajwa kuwa mwanamitindo maarufu nchini Marekani.

Juzi wakati wa kuadhimisha siku ya wanawake duniani, Bieber, alionekana ‘akiposti’ picha nyingi za mpenzi wake huyo na kuzua gumzo mitandaoni kuwa mwanamuziki huyo raia wa Canada anamuumiza roho, Selena Gomez.

Selena ambaye alikuwa mpenzi wa zamani wa Bieber, alidai kuwa staa huyo hatapata mwanamke kama yeye sababu alikuwa akimpenda kwa dhati.

Hata hivyo, imebainika kuwa Bieber yupo tayari kufunga ndoa na Baldwin mwenye umri wa miaka 22 na hivi karibuni wamekuwa wakionekana pamoja maeneo tofauti tofauti wakila bata.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here