Home Habari Bodi ya Filamu yasema Wema Sepetu bado yupo kifungoni, hajafunguliwa

Bodi ya Filamu yasema Wema Sepetu bado yupo kifungoni, hajafunguliwa

3231
0
SHARE

Elizabeth Joachim

Katibu mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini, Joyce Fissoo amesema msanii wa filamu, Wema Sepetu hajafunguliwa kujihusisha na masuala ya uigizaji kama inavyovumishwa mitandaoni.

Katibu huyo ameeleza hayo leo Jumatano Januari 9 katika Ofisi za Baraza hilo Jijini Dar es Salaam alipokuwa na mkutano na waandishi wa habari.

Amesema endapo msanii huyo atafunguliwa Baraza hilo litaitisha mkutano na waandishi wa habari kwa ajili ya kulieleza jambo hilo na si kama inavyoelezwa kwenye mitandano ya kijamii.

“Jamani naombeni muachane na stori za mitandaoni, Wema bado yupo kifungoni na endapo itatokea akaruhusiwa kujihusisha na masuala ya uigizaji bodi itaitisha mkutano na wandishi wa habari na kila mtu atajua,” ameeleza Joyce

Wema Sepetu amefungiwa na bodi hiyo Oktoba 26 mwaka jana kwa kosa la kusambaa mitandanoni kwa video yake chafu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here