Home Habari Bondia Majiha amtunishia msuli Kimweri

Bondia Majiha amtunishia msuli Kimweri

1415
0
SHARE

NA GLORY MLAY

BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini, Fadhili Majiha, amesema kwa mazoezi aliyofanya anaamini atamwangusha mpinzani wake, Patrick Kimweri kutoka Tanga katika raundi ya kwanza, katika pambano lisilo la ubingwa litakalofanyika Iddi Pili, Manzese jijini Dar es Salaam.

Pambano hilo linatarajiwa kuwa la raundi 10, katika uzani wa Kg 53.5.

Akizungumza na DIMBA Jumatano, Majiha, alisema anaendelea na mazoezi kwani anaamini pambano hilo litakuwa la ushindani lakini atashinda katika raundi ya pili.

“Mpinzani wangu ninamfahamu hivyo sina haja ya kulumbana naye kwani nitamlambisha sakafu raundi ya pili kikubwa naomba mashabiki wajitokeze kwa wingi ili kushuhudia burudani.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here