Home Burudani Katy Perry auza jumba lake bil 21/-

Katy Perry auza jumba lake bil 21/-

1515
0
SHARE


WASHINGTON, Marekani

STAA wa muziki wa Pop nchini Marekani, Katy Perry, amefanikiwa kuuza jumba lake lililopo kwenye miinuko ya Hollwood kwa dau la pauni milioni 7 (bilioni 21.4 za Tanzania).

Inadaiwa kuwa jumba hilo kubwa lilikuwa sokoni kwa miaka miwili na nusu, lina vyumba zaidi ya 10 huku pia, kukiwa na ukumbi wa kuangalia sinema, bwawa la kuogelea, sehemu ya kufanyia mazoezi na jiko la kupikia pizza.

Inatajwa kuwa mnunuzi ni Michael Chow, ambaye ni mmoja wa wafanya biashara wakubwa nchini Marekani, pia ni mwanzilishi wa maduka ya Mr. Chow ambayo yanasimamiwa na mke wake, Vanessa Rano.

Perry aliinunua nyumba hiyo mwaka 2013 lakini aliamua kuiuza baada ya kuchumbiwa na mpenzi wake wa muda mrefu, Orlando Bloom, ambao wanaishi pamoja.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here