Home Habari TBF bado wanateswa na ubovu wa uwanja

TBF bado wanateswa na ubovu wa uwanja

1386
0
SHARE

NA GLORY MLAY

RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), Pharesi Magesa, amewataka wadau kuendelea kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kusapoti Ligi ya Mkoa wa Dar es Salam na ukarabati wa Uwanja wa Ndani wa Taifa, jijini hapa.

Akizungumza na DIMBA Jumatano, Magesa, alisema wanahitaji kupata sapoti ya kutosha kuhakikisha ligi hiyo inafanikiwa na mshindi anapatikana kihalali.

Alisema tatizo la uwanja kujaa maji limeendelea kuathiri RBA kwani wachezaji wanashindwa kucheza hivyo wadau wajitokeze kwa ajili ya kutoa sapoti ya ujenzi. “Ligi inaendelea lakini bado tunahitaji wadhamini wakutosha kuhakikisha mwaka huu zawadi zinaboreshwa na uwanja wa ndani unakamilika hivyo tunawaomba wajitokeze kwa ajili ya kuendelea kukuza mchezo huu hapa nchini kwa kupata wachezaji bora,” alisema

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here