Home Dondoo za Ulaya MAHOJIANO YA KWANZA YA MATIC NDANI YA UNITED

MAHOJIANO YA KWANZA YA MATIC NDANI YA UNITED

596
0
SHARE

MANCHESTER, England

MUDA mfupi baada ya kutangazwa kuwa mchezaji wa Manchester United, Nemanja Matic, alifanikiwa kufanya mahojiano yake ya kwanza na kituo cha Televisheni cha timu hiyo, MUTV.

Mahojiano hayo yaligusa sehemu mbalimbali huku akimtaja Jose Mourinho kuwa mtu aliyemvutia zaidi kujiunga naye tena kufanya kazi na Mreno huyo kwenye kikosi hicho.

SWALI: Nemanja, awali ya yote karibu Manchester United. Unajisikiaje kuwa mchezaji wa timu hii?

MATIC: Najisikia vizuri. Manchester United ni moja ya timu kubwa duniani, najisikia furaha kuwa sehemu ya timu hii. Ninachosubiri sasa ni kuanza mazoezi pia kucheza mechi nikiwa kwenye jezi ya United.

SWALI: Umeondoka timu ambayo imeshinda kombe msimu uliopita. Kipi kilichokufanya ujiunge na Manchester United?

MATIC: Kama nilivyosema, Man United ni timu kubwa duniani. Pia kufanya mazoezi chini ya Mourinho tena ni jambo bora kwangu, kuwa na kocha kama yeye ni jambo la kipekee. Hauhitaji kufikiria sana kuhusu hilo. Jose na Manchester si vitu vya kufikiria sana.

SWALI: Unajisikiaje kufanya kazi chini ya Mourinho tena?

MATIC: Najisikia furaha kufanya naye kazi tena, ni kocha mkubwa sana. nimefanya naye kazi kabla, muda mwingi amekuwa akinisaidia kuwa bora kila wakati. Nafurahi kuungana naye tena, hasa katika timu kubwa duniani.

SWALI: Hii ni mara ya pili unasajiliwa na Mourinho, unajisikiaje jinsi anavyokupa thamani katika kazi yake?

MATIC: Kwangu ni furaha sana. Inanipa hamasa katika ufanyaji kazi wangu, pamoja na uwezo zaidi. Nitajaribu kuonyesha uwezo wangu wote ili nionekane nilistahili kuwa sehemu ya timu hii.

SWALI: Unajisikiaje kukamilisha usajili kabla ya msimu kuanza, ili ujuane na wachezaji wenzako?

MATIC: Ni jambo bora kuingia timu mpya mapema. Inasaidia kujua mipango ya kocha mapema, pia inasaidia kujuana na wachezaji. Nafurahi nitakuwa na muda wa kufanya nao mazoezi kabla ya mchezo wangu wa kwanza dhidi ya Real Madrid. Hakika msimu huu tutafanya mambo makubwa tukiwa pamoja.

SWALI: Ulikuwa ukifanya mazoezi na Chelsea, lakini hukucheza mchezo hata mmoja wa ‘pre-season’. Inakusaidiaje kuwa imara katika msimu mpya?

MATIC: Kama ulivyosema, sikubahatika kufanya mazoezi na timu zaidi ya kuwa peke yangu na kocha wa ‘fitness’ tu. Kufanya mazoezi mwenyewe bila timu huwa inakuwa tofauti. Muda bado ninao wa kufanya mazoezi na wenzangu. Siko sawa 100% lakini nitakuwa sawa hivi karibuni.

SWALI: Unajua nini kuhusu usajili wetu wa kwanza, Lukaku (Romelu) na Lindelof (Victor)? Hasa Lindelof ambaye ametoka Benfica kama wewe.

MATIC: Ndio, nawajua wote. Victor tulikuwa pamoja Benfica, lakini Lukaku sikupata nafasi ya kucheza naye sababu wakati mimi naondoka Chelsea, yeye alisaini miaka mitatu, lakini namfahamu vizuri sababu nimekuwa nikicheza dhidi yake mara kwa mara. Wote wawili ni wachezaji wazuri, wataisaidia Man United kufika kwenye malengo.

SWALI: Umeshinda makombe mawili ya Premier League na Chelsea, unadhani kikosi hiki cha Man United kipo tayari kufanya hivyo?

MATIC: Nadhani kipo tayari kwa sababu wachezaji wamekwishapevuka. Wamefanya kazi na Jose kwa mwaka mmoja, naamini sasa wanajua majukumu yao. Naamini msimu huu watafanya mambo mengi mazuri.

SWALI: Unajizungumziaje wewe mwenyewe kama mchezaji. Kipi kinakufanya kuwa bora?

MATIC: Ni ngumu kusema kuhusu hilo. Nawaachia mashabiki wazungumze kuhusu mimi. Lakini kama nilivyosema nitafanya kazi yangu vizuri, nitajaribu kufanya hivyo. Ila nawaachia mashabiki waseme kuhusu ubora wangu.

SWALI: Umecheza dhidi ya Man United hapa Old Trafford mara kadhaa, unajisikiaje utakapovaa jezi nyekundu mbele ya mashabiki 70,000?

MATIC: Ni kitu spesho kwangu, kucheza Old Trafford nikiwa na jezi nyekundu. Itakuwa siku nzuri kwangu, ndio ni jambo ambalo nalisubiri kwa hamu kubwa.

SWALI: Mwisho, una ujumbe wowote kwa mashabiki wa United duniani kote?

MATIC: Tutafanya kila kitu kuwafanya wawe na furaha kwa kushinda kombe la ligi msimu huu. Ndio, tutafanya hivyo, tutatoa tulichonacho zaidi ya 100%.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here