SHARE

NA JESSCA NANGAWE


BAADA ya mwishoni mwa juma staa wa filamu, Wema Sepetu kuzindua filamu yake mpya ya ‘Heaven Sent’, mwigizaji mwenzake, Aunt Ezekiel, amefunguka na kudai ujio wa filamu hiyo utaleta mapinduzi mapya katika tasnia hiyo.

Wema alizindua filamu yake hiyo katika ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam, ambao ulihudhuriwa na watu mbalimbali, wakiwamo wasanii wenzake.

“Ukweli Wema ameonyesha bado BongoMovie ipo na inafanya vizuri, nadhani ujio wa kazi yake hii utaongeza hamasa na kuleta mapinduzi katika tasnia hii ya filamu, namuombea aendelee kufanya vizuri na asiishie hapa, kwani safari yetu bado ni ndefu,” alisema Aunt Ezekiel.

Alisema wapo mastaa wanaopika kazi zao, ikiwamo yeye, hivyo mashabiki zake wakae mkao wa kula, kwani wakati wowote atakuja na igizo jipya ambalo anaamini litafanya vyema kwenye soko la filamu ndani na nje ya Tanzania.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here