SHARE

arda turanBARCELONA, Hispania

KIUNGO wa Barcelona, Arda Turan, amerusha kijembe kwa klabu ya Arsenal akisema kuwa angeichezea klabu hiyo kama asingekuwa kwenye kiwango bora.

Turan alisajiliwa na Barca kutoka Atletico Madrid msimu uliopia lakini alianza kuitumikia klabu hiyo, Januari mwaka huu baada ya Wakatalunya hao kumaliza kifungo chao cha kutosajili.

“Nilikuwa na fikra za kusajiliwa Barca,” alisema Arda. “Ukweli ni kwamba, nilikuwa nikiamini kama nikicheza kwa juhudi nitasajiliwa Barca, lakini kama nikicheza kawaida tu ningeishia kuwa mchezaji wa Arsenal.”

“Mimi napenda kucheza na mpira kwa urahisi zaidi. Lakini si hivi tu, nataka nicheze kwenye kiwango bora. Hivyo nafikiri sikuja hapa Barca kwa bahati mbaya,” aliongeza kiungo huyu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here