SHARE

NA MAREGESI NYAMAKA

RASMI Juni 21 mwaka huu michuano ya Kombe la Mataifa Afrika (Afcon 2019) itakuwa inaanza kutimua vumbi katika mji wa Cairo mchezo wa ufunguzi ukiwakutanisha wenyeji Msiri dhidi ya Zimbabwe.

Katika michuano hiyo moja kati ya mataifa ambayo ni wageni baada ya kupita miaka kadhaa ni Tanzania (Taifa Stars) waliokuwa watazamaji zaidi ya miaka 30 iliyopita.

Tayari kocha wa kikosi hicho, Emmanuel Amunike ameanza kulifua jeshi lake hilo lenye jumla ya wanaume 32 na baadaye utafanywa mchujo na kubaki 23 wakaopata nafasi ya kwenda Misri.

Stars ambao wapo kundi C wanatarajia kushuka dimbani Juni 23 kuvaana na Senegal alipo strika matata kutoka Liverpool, Sadio Mane kabla ya kuwavaa majirani Kenya Juni 30, huku mchezo wa mwisho katika hatua ya makundi ukiwakutanisha na Algeria.

Kama ilivyo kawaida ya DIMBA gazeti pendwa la watu kila Jumatano kupitia ukurasa huu litakuwa linakuletea mambo kadhaa kutoka kwa wachezaji wa zamani wa Stars, wachambuzi wa soka, lakini pia wasemavyo mashabiki pamoja kinachoendelea Misri.

Kona ya shabiki

Deus Ladslaus ëBaba la Babaí shabiki wa Taifa Stars anasema yeye ni mombi/dua kila kukicha kuwaombea wachezaji na benchi lake la ufundi, lakini pia akiwataka Watanzania kuacha kuwaofia Senegal na Algeria.
ìHakuna kundi gumu wala jepesi, wakati ugumu tunautengeneza wenyewe, naamini wachezaji wangu wakiongozwa na miongoni mwa mastraika bora Ulaya kwa sasa Mbwana Sammatta.î Anasema.

Vinywa vya wakongwe

Mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa Starsm Adolf Rishald ambaye kwa sasa ni kocha wa timu ya Tanzania Prisons anasema maandalizi bora yanazaa kilicho bora.

Jambo la kwanza ni maandalizi bora, lakini pia makundi yamepangwa mapema kocha anawatambua wapinzani, kingine mashabiki wasiwatwishe mzigo mkubwa wachezaji,î anasema.

Kwa upande beki wa kushoto wa zamani wa kikosi hicho Leopard Taso ëMtebezií anaeleza kwamba nidhamu inabeba vyote kuanzia kwenye maozoezi kumsikiliza kocha hadi kwenye michuano yenyewe
ìHaya ni mashidano, sijaona kama timu imechelewa sana ilifanya maandalizi, nasikia tutawahi kuwasili Misri mapema itatusaidia wachezaji kuzoa hali ya hewa, lakini pia mechi ya kirafiki watakayocheza na Misri itatusadia sanaî.

Pia lile kitu kuitwa ëunder dogí siku hizi halina nafasi ukishangia kwenye mashindano kila kitu kinakuwa sawa hakuna kusema huyu ni Senegal, hawa wana Wanyama (Victor) haipo,îanasema.

Nigeria wapiga mkwara

Baada ya Nigerai kusua sua kwenye michuano kadhaa huko nyuma, mchezaji wa zamani wa Taifa hilo, Joseph Yobo anadai watafanya makubwa mwaka huu.

Yobo mwenye umri wa miaka 38 aliyewahi kuichezea Everton ya England aliliambia BBC Sports kuwa, timu yao itawangaza wengi nchi Misri ikiwezekana kutwaa taji hilo.

Hili Taifa kubwa ambalo lina watu zaidi ya Mil 200, tufanya kitu wachezaji wetu wanatambua dhamana waliyoibeba.

Ghana kama wote

Tayari timu ya Taifa Taifa ya Ghana ëBlack Starsí wapo katika jiji la Abu Dhabi walipowasili mwishoni mwa wiki wakiendelea kujifua chini ya kocha wao mzawa, Kwesi Appiah.

Mbali na kujifua mazoezini pia watakuwa na mechi mbili za kirafiki ili kujiweka sawa, watacheza Juni 10 dhidi ya Afrika Kusini kabla ya kutua Misri Juni 20 siku tano kabla ya kuanza kivumbi kwenye kundi la F walipo Guenea-Bissau, Cameroon na Benin.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here