Home Habari AFRICAN LYON YASHUSHA KOCHA MFARANSA, STRAIKA

AFRICAN LYON YASHUSHA KOCHA MFARANSA, STRAIKA

6480
0
SHARE

 NA MAREGES NYAMAKA                |         


WAKATI African Lyon ikiwa haizungumzwi sana na wadau wa soka, wenyewe wameamua kufanya mambo yao kimyakimya na jana wameshusha bonge la kocha kutoka nchini Ufaransa.

Kocha huyo alikuwa anatarajiwa kutua na straika matata, Victor da Costa, ambaye unaambiwa uwezo wake utawafanya mabeki wa timu pinzani kukosa usingizi.

Kigogo mmoja wa timu hiyo aliliambia DIMBA kuwa, walikuwa Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere kusubiri wageni wao hao.

“Hivi sasa tunavyozungumza (jana) tupo Uwanja wa Ndege tukimsubiri kocha Mfaransa kuungana nasi, lakini hatakuwa mwenyewe, ameambatana na straika, Victor da Costa, ambaye tayari jina lake lipo kwenye usajili wetu wa hasa ile orodha ya wachezaji wa kigeni,” alisema mpenyeza taarifa.

Kigogo huyo alikataa kulitaja jina la kocha huyo, akidai aulizwe Mkurugenzi wa timu hiyo, Rahim Kangezi, maarufu kama Zamunda, ambaye hata hivyo alikataa kutoa ushirikiano.

Zamunda alipoulizwa juu ya kocha huyo alisema ingekuwa busara kufanya utafiti wa namna Klabu zitakavyopata wadhamini kuliko kutafuta habari nyingine.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here