Home Michezo Afrika AFYA YA JORDAN AYEW YAIMARIKA

AFYA YA JORDAN AYEW YAIMARIKA

529
0
SHARE

LONDON, England

NYOTA wa timu ya taifa ya Ghana, Jordan Ayew, afya yake imezidi kuimarika  ambapo imeelezwa anaweza kuanza tena kuitumikia klabu yake ya Swansea City, ikiwa ni muda mfupi baada ya kukosa mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia mwaka 2018, dhidi ya Brazzaville Jumanne iliyopita.

Ayew (25), alishindwa kusafiri na Ghana kwenda kuivaa Congo baada ya kuumia, ambapo timu hiyo iliibuka na ushindi ugenini wa mabao 5-1, ambapo hivi sasa taarifa kutoka kwenye klabu yake zinasema kwamba yupo kwenye hali nzuri na kwamba anaweza kuanza kuitumikia timu yake wakati wowote.

Mwenyewe Ayew amesema kwamba, anashukuru wenzake kufanikiwa kupata ushindi mnono kwenye ardhi ya ugenini, jambo lililompa faraja, ingawa kwa sasa yupo tayari kwa mapambano mapya.

“Jambo la muhimu ilikuwa ni timu kupata ushindi, hilo limefanyika, kwa hiyo binafsi nimefarijika kuona namna mambo yanavyokwenda ndani ya Ghana kwa sababu imetoa changamoto ya kupambana zaidi na kuongeza juhudi ili kupata ushindi na kwenda Kombe la Dunia,” amesema nyota huyo.

Ghana ipo Kundi E, lenye timu za Misri, yenye pointi tisa baada ya kucheza mechi nne, huku Uganda ikishika nafasi ya pili baada ya kucheza mechi nne kukusanya pointi saba.

Ghana inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi tano, baada ya kucheza nne na Congo ikishika mkia baada ya kucheza nne na kupata pointi moja.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here