SHARE

download (2)

NA CLARA ALPHONCE

MECHI ya watani wa jadi itayowakutanisha Simba na Yanga siku ya Jumatano ijayo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, huenda ikaharibu vibarua vya makocha wao, George Lwandamina (Yanga) na Joseph Omog (Simba).

Tayari kumekuwa na maneno mengi juu ya vibarua vya makocha hao, kutokana na viwango vya timu zao katika mechi za majaribio, kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kocha Lwandamina anaweza kuondoka Yanga endapo atapoteza mchezo huo, kwani tayari amekwisha kufungwa na Simba mara mbili, kwenye Kombe la Mapinduzi ambapo alifungwa kwa penalti 4-2 na mchezo wa mwisho wa ligi.

Hata hivyo, Mzambia huyo tayari amemaliza mkataba na klabu hiyo, ila viongozi wanasita kumpa mkataba mpya kwa kile kinachodaiwa kwamba, inasubiriwa mechi dhidi ya Simba ipite.

Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa, alikiri kocha huyo kumaliza mkataba wake wa awali wa miezi sita na muda wowote watapewa mkataba mpya, bila kueleza ni lini hasa zoezi hilo litakamilika.

Kwa upande wa Omog, mashabiki wamekwishaanza kumpigia kelele, kwa madai kuwa mfumo anaotumia unaikosesha timu mabao pamoja na kuwa na wachezaji wengi wazuri msimu huu.

Mechi ya Ngao ya Jamii mara kadhaa imekuwa ni tabu kwa makocha, kutokana na kuamua hatima ya vibarua vyao, kutokana na historia ya timu hizo.

Baadhi ya makocha ambao walifukuzwa baada ya kumalizika kwa mechi hizo na kufungwa ni Ernie Brandts, raia wa Uholanzi aliyekuwa akiifundisha Yanga, Zdravko Logarusic kutoka Croatia na Mzambia Patrick Phiri, waliokuwa wakiifundisha Simba.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here