Home Habari AISHI MANULA APATA JIKO

AISHI MANULA APATA JIKO

976
0
SHARE
NA JESSCA NANGAWE

KIPA namba moja wa Simba, Aishi Manula, ameuaga ukapera baada ya kufanikiwa kufunga pingu za maisha na aliyekua mpenzi wake wa muda mrefu.

Aishi alifunga ndoa hiyo juzi Ijumaa na mpenzi wake aitwaye Aisha, mkoani Morogoro.

Kutokana na kuwa kwenye majukumu hayo, Aishi ameshindwa kuungana na wenzake ambao wapo kwenye mashindano ya Kombe la Mapinduzi yanayoendelea visiwani Zanzibar.

Taarifa zinaeleza, Aishi na Aisha, wamekuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi kwa muda mrefu kabla ya kuchukua uamuzi wa kuwa mke na mume.

Manula si kwamba ni kipa namba moja wa Simba peke yake, bali pia ni tegemeo kwenye kikosi cha timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ na sasa anachukuliwa kama ‘Tanzania One’, kutokana na uwezo wake anaposimama langoni.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here