Home Habari AJIB: SINGIDA ACHENI MANENO, WEKENI MUZIKI

AJIB: SINGIDA ACHENI MANENO, WEKENI MUZIKI

568
0
SHARE

NA SAADA SALIM,

STRAIKA wa Simba, Ibrahim Ajib, amesikia jina lake likitajwa katika usajili wa klabu ya Singida United wakati bado hawajaafikiana na sasa ameamua kuwapasukia viongozi wa timu hiyo kwamba waache maneno na badala yake waweke mezani dau analolitaka.

Kwa wiki kadhaa sasa Ajibu amekuwa akihusishwa kumwaga wino Singida United, iliyopanda daraja msimu huu ikiwa chini ya aliyekuwa kocha wa Yanga, Hans Pluijm, ikielezwa anatakiwa kwa udi na uvumba kwenye kikosi cha timu hiyo.

Akizungumza na DIMBA Jumatano, Ajib alisema, suala la Singida kumhitaji halina pingamizi, kutokana na kupokea simu nyingi kutoka kwa viongozi na benchi la ufundi la timu hiyo, wakiongozwa na Pluijm, lakini bado hawajaafikiana.

Alisema ameshachoshwa na simu nyingi, kwa sasa anahitaji kuona timu hiyo ama nyingine ambayo inamhitaji kuweka mzigo wa maana mezani ili asaini.

“Ni kweli napokea simu nyingi kutoka Singida, sasa zinachosha, kama vipi waweke dau ambalo nalihitaji mezani nimwage wino,” alisema.

Ajib alisema tangu amewatajia kiasi ambacho anakihitaji bado hawajamjibu, zaidi ya kumpigia simu za kumuahidi kwamba wako katika malengo naye.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here