KIUNGO wa Bayern Munich, Thiago Alcantara, amesema kuwa anayafurahia maisha ya Ujerumani, lakini yuko tayari kurejea Barcelona, kama akihitajika.
Alcantara alitua Munich, mwaka 2013 na kuwa mchezaji muhimu kwenye kikosi cha wababe hao wa Bundesliga.