Home Michezo Kimataifa ALDRIDGE: LIVERPOOL INGIENI SOKONI KUSAKA ‘STRAIKA’

ALDRIDGE: LIVERPOOL INGIENI SOKONI KUSAKA ‘STRAIKA’

434
0
SHARE

MERSEYSIDE, Liverpool

MAJOGOO wa Anfield, klabu ya Liverpool, imekosa nafasi ya kujikita ndani ya ‘Top Four’ kwa tofauti nzuri ya pointi dhidi ya wapinzani wake, Man City, Arsenal na Man United, baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na Man City, mchezo uliochezwa mapema wikiendi iliyopita.

Nafasi nyingi zilitengenezwa na vijana hao wa kocha Jurgen Klopp, lakini zilishindwa kutumika ipasavyo, na ndiyo maana mkongwe wa zamani wa Liverpool, John Aldridge, anasema Klopp hana budi kusajili mtambo wa mabao kwenye dirisha lijalo la usajili.

“Liverpool inahitaji straika ambaye ni ‘top class’, hivyo Klopp atumie fedha.

“Ule mchezo wa City, wakati Liver ikiwa na bao moja la kuongoza ilikuwa tayari imeshaumiliki mchezo, je, nani wa kumalizia nafasi zinazotengenezwa? Angalau Roberto Firmino na Adam Lallana wangeweza kuipa timu pointi tatu, lakini umaliziaji bado,” alidai Aldridge.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here