Home Michezo Kimataifa AMECHANGANYIKIWA

AMECHANGANYIKIWA

8480
0
SHARE

MERSEYSIDE, England

Daktari asema Karius hayupo sawa kiakili, Madrid wahusika


IMEBAINIKA kuwa kipa wa Liverpool, Loris Karius, hayupo sawa kiakili tangu timu hiyo ilipokubali kichapo cha mabao 3-1 katika mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid.

Katika mchezo huo, Karius alifanya makosa mawili yaliyoipa mabao Real Madrid, lakini hata mchezo ulipomalizika alionekana akiomba msamaha kwa mashabiki wa Liverpool.

Kipa huyo alikuwa kwenye kiwango kizuri katika michezo yote ya Ligi ya Mabingwa ambayo alicheza isipokuwa siku hiyo ya fainali.

Mapema wiki hii jopo la madaktari wa Liverpool walimfanyia vipimo kipa huyo nchini Marekani na kugundua anasumbuliwa na msongo wa mawazo ambao unaweza kumpelekea ashindwe kufanya vizuri awapo uwanjani.

“Mr. Karius anasumbuliwa na mawazo ambayo yanaweza kuathiri kiwango chake uwanjani, anahitaji kuhudhuria kliniki ya ushauri ili arudi katika hali yake,” alisema dokta.

Naye Karius alisikika akisema anatamani mchezo huo urudiwe tena ili afute makosa yake.

“Najua nimefanya makosa mawili makubwa katika mchezo ule, natamani urudiwe ili nifute makosa yangu,” alisikika kipa huyo

 

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here