Home Habari Amunike aipa simba ubingwa wa Afrika

Amunike aipa simba ubingwa wa Afrika

2435
0
SHARE

NA TIMA SIKILO

KOCHA mkuu wa timu ya Taifa ‘Taifa Stars’, Emmanuel Amunike, amekiangalia kwa umakini kikosi cha Simba namna kilivyo sheheni wachezaji wenye uwezo mkubwa kisha akajikuta akitamka wazi kwamba wanaweza kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Wekundu hao wa Msimbazi, wanatarajiwa kuondoka leo kwenda Zambia kukipiga na Nkana mchezo wa kwanza ambao utachezwa Desemba 15, nchini humo kabla ya mchezo wa marudiano Desemba 22 mwaka huu Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na DIMBA Jumatano, Amunike alisema Simba ni moja ya timu kubwa Tanzania na ina uwezo wa kufanya makubwa katika michuano hiyo ya Afrika na hata kutwaa ubingwa.

“Simba ni timu kubwa sana hapa Tanzania, ninauhakika watafanya mambo makubwa katika michuano hiyo ya Afrika na binafsi nadhani halitakuwa jambo la kushangaza wakitwaa ubingwa.”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here