SHARE

MERSEYSIDE, England

KOCHA wa Everton, Carlo Ancelotti, amekiri kuwa Liverpool walifanya uamuzi sahihi kumnyima kazi na kumwajiri Jurgen Klopp.

Ancelotti mwenye umri wa miaka 60 amedai kuwa aliwahi kutakiwa na Liverpool mwaka 2015 lakini ghafla walimpa kisogo na kumchukua Klopp aliyekuwa Borussia Dortmund.

Kauli ya Ancelotti imekuja kuelekea mchezo wao dhidi ya Liverpool utakaochezwa leo pale Anfield, ambao ni wa raundi ya tatu ya Kombe la FA.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here