SHARE

MADRID, Hispania

UHAMISHO wa Antoine Griezmann kutoka Atletico Madrid kwenda Barcelona uliyokamilika siku kadhaa zilizopita umetoa taswira mpya katika safu ya ushambuliaji ya mabingwa hao wa La Liga.

Griezmann anakuwa mchezaji wa nne kusajiliwa na Barcelona katika katika kipindi hiki cha dirisha kubwa baada ya kiungo, Frenkie de Jong kutoka Ajax, golikipa Neto kutoka Valencia na beki Emerson kutoka klabu ya Atletico-MG ya Brazil.

Uwezo wake wa kuwatungua makipa na  kiasi kikubwa cha pesa Euro milioni 120  walichotoa Barcelona inaelezwa inamfanya kuwa na nafasi kubwa ya kuanza kikosi cha kwanza.

Hatua hiyo unakifanya kikosi hicho kuwa na utatu wa Lionel Messi ambaye ana namba ya kudumu, mtambo mwingine wa mabao, Luis Suarez  sambamba na Griezman mwenyewe(MSG).

Mbali na Mshindi huyo wa Kombe la Dunia akiwa na timu taifa ya Ufaransa mwaka uliyopita  kuwekewa kipingepele na klabu yake hiyo mpya kwamba  kwa klabu itakayomuhitaji itahitajika kutoa kitita cha Euro milioni 800, haya hapa mambo mengine matano usiyoyajua.

Usiyoyajua kuhusu Griezmann?

Umbo dogo lamponza

Licha mafamikio makubwa aliyonayo sasa, lakini amekumbana na changamoto kadhaa akiwa tangu mdogo ikiwamo kukataliwa na academy  kadhaa kutokana na umbo lake dogo wakati huo.

Miongoni mwa klabu hizo ni Lyon, huku ikielezwa pia afya yake haikuwa  inaridhisha sana kujiunga na watoto wenzake kwenye accemy hiyo.

Beckham, Sliva  ndo ‘mafundi’ wake

Griezmann tangu akiwa mdogo alikuwa anavutiwa zaidi na aina ya soka la straika wa zamani wa Manchester United na timu ya taifa ya England, David Robert Joseph Beckham pamoja na kiungo wa Manchester City, David Silva.

Kwa upande wa mchezo wa kikapu, anaoupenda na kuufuatilia  kwa karibu hasa  Ligi Kuu Marekani (NBA) anavutiwa zaidi na Derrick Rose wa Detroit Pistons.

Amuweka ‘mfukoni’ Messi

Griezmann ndiye mchezaji pekee aliyeafanikiwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi mara mbili katika msimu mmoja akifanya hivyo Januari, 2015  pamoja na  April, huku Messi yeye akifanya hivyo mara moja Januari 2016.

Nyumbani kwake kuna  uwanja wa kikapu

Mshindi huyo wa  Kombe la Europa, Super Cup la , pamoja na Uefa Super Cup akiwa na Atletico Madrid nyumbani kwake katika jiji la Madrid kuna uwanja wa mpira wa kikapu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here