SHARE

CATALUNYA, HISPANIA

KOCHA mkuu wa klabu ya FC Barcelona, Ernesto Valverde, amesema kuwa atampa mechi nyingi zaidi mshambuliaji mpya wa timu hiyo Antoine Griezmann ili kumuweka sawa mara baada ya kikosi chake kupoteza mechi ya ufunguzi  wa Ligi kwa kukubali kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Athletic Bilbao.

Griezmann amejiunga na Barca akitokea Atletico Madrid kwa dau la Euro milioni 120 katika majira haya ya usajili mchezo wake wa kwanza ameanza katika dimba la San Mames.

Katika mtanange huo nyota huyo alikuwa akihaha kuonyesha ubora wake akitokea upande wa kushoto katika watu watatu wa safu ya ushambuliaji lakini baada ya Luis Suarez kupata majeraha akalazimika kubadilishwa na kucheza kama mshambuliaji wa kati.

“Kama angekuwa ndani ya boksi angeweza kumalizia, anaanza vyema, lakini anapaswa kuuchukua mchezo . “Kumuweka upande wa kushoto tunajua atakuwa akilitazama goli,lakini tuna mabeki wa pembeni ambao pia wanaweza kuuchukua mchezo,” alisema Valverde

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here