Home Michezo Kimataifa ANTONIO CONTE: TUTAPIGA KILA ATAKAYEKATIZA MBELE YETU

ANTONIO CONTE: TUTAPIGA KILA ATAKAYEKATIZA MBELE YETU

496
0
SHARE

LONDON, England

ANTONIO Conte anaamini kichapo cha bao 3-0 Chelsea walichokitoa kwa Bournemouth kimetosha kufikisha ujumbe kwa wapinzani wao kuwa wako ‘siriaz’ na ubingwa na wanaweza kupata ushindi hata bila ya nyota wao.

“Nafikiri tumetuma ujumbe mzuri kwa wapinzani wetu,” alisema kocha huyo wa Chelsea aliyeiongoza klabu hiyo kuweka rekodi ya kushinda mechi 12 mfululizo kwenye Premier League.

“Watu wengi walikuwa wakisubiri kuona kama tutapoteza tukicheza bila wachezaji wetu muhimu, Diego Costa na N’Golo Kante lakini haikuwa hivyo, niwapongeze wachezaji wangu na hii ni ishara kuwa tuna kikosi imara zaidi msimu huu.”

Chelsea kwa sasa wanaifukuzia rekodi ya Arsenal ya kushinda michezo 14 ya ligi mfululizo ambao pambano lijalo watacheza na Stoke City.

“Nina imani tutaendelea na moto huu mpaka mwisho wa msimu,” alijibu Conte, akijibu swali aliloulizwa kama Chelsea wana uwezo wa kushinda mechi zote za ligi.

“Rekodi hazina umuhimu wowote kama hutapata mafanikio mwisho wa msimu. Jambo muhimu kwetu kwa sasa ni kuangalia msimamo utakavyokuwa, haijalishi tumeshinda 12 au 36.

“Tunajivua kuwa na rekodi hii na tunataka tuendelee kushinda mechi zetu lakini tuna uhakika kuwa haitakuwa rahisi kama tunavyofikiria. Hapa kila mechi ina ugumu wake na dhidi ya Stoke tutaona hiki ninachokisema.”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here