Home Michezo Kimataifa Arsenal mnamtaka Icardi? Andaeni hela ya Pogba

Arsenal mnamtaka Icardi? Andaeni hela ya Pogba

424
0
SHARE

INTER Milan wameipasha klabu ya Arsenal kuwa kama wanataka kumsajili straika wao, Mauro Icardi, basi ni lazima waweke mezani kitita cha pauni milioni 99.

Kiasi hiki kimewekwa kama sehemu ya kuvunja mkataba wake hivyo Wenger anatakiwa kujilipua kama kweli anaihitaji huduma ya straika huyu wa kimataifa kutoka Argentina.

 

Juventus yatoa sharti la kumtoa Bonucci

HATIMAYE klabu ya Juventus imesema kuwa wapo tayari kumwachia mlinzi wao, Leonardo Bonucci (29), kujiunga na Chelsea endapo watalipwa pauni milioni 50 na Cesc Fabregas.

Juventus wametoa tamko hilo hasa baada ya kocha wa Chelsea, Antonio Conte, kuonyesha nia ya dhati ya kumhitaji Bonucci ikiwa ni sehemu ya kuiimarisha safu yake ya ulinzi.

 

Aubameyang aziingiza vitani City na Chelsea

CHELSEA na Manchester City wameanza mbio za kuiwania saini ya straika hatari wa Borussia Dortmund, Mgabon Pierre Emerick-Aubameyang.

Aubameyang (27), ameshathibitisha kuwa ataondoka Dortmund msimu ijao na dau lake linatajwa kuwa ni pauni milioni 65.

 

Leicester wabeba straika wa mtaani

MABINGWA watetezi wa Premier League, Leicester City, wamemchukua kwa majaribio straika wa klabu ya mtaani Harrow Borough, Ibrahim Meite.

Meite (20) anajulikana kwa jina la utani la ‘The Shark’, amefunga mabao 10 kwenye michezo yake ya mitaani aliyocheza msimu huu.

 

England wajiongeza kwa dogo Dembele

CHAMA cha Soka nchini England (FA), kimeanza mazungumzo na wazazi wa dogo wa miaka 13, Karamoko Dembele, kwa ajili ya kumpa uraia wa taifa hilo.

Dembele ni raia wa Scotland na zao la akademi ya Celtic na alivuma sana mitandaoni baada ya kupangwa kwenye kikosi cha vijana cha U-20 huku akiwa na umri mdogo.

 

Unamkumbuka Zaza? Sikia anachowafanya West Ham

WEST Ham watalazimika kuilipa Juventus pauni milioni 20 endapo straika, Simone Zaza (25), atacheza mechi nyingine 10 akiwa na wagonga nyundo hao wa jiji la London.

Juventus waliingia mkataba na West Ham wa kulipwa pesa kamili endapo watamtumia Zaza kwa michezo zaidi ya 14.

 

Begovic aamua kukomaa Chelsea

KIPA Asmir Begovic (29), amekubali kubaki na kuendelea kugombea namba katika kikosi cha Chelsea.

Begovic amekuwa chaguo la pili nyuma ya Thibout Courtouis, ametoa maamuzi hayo baada ya kuombwa na Conte kubaki darajani.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here