Home Uchambuzi Arsenal si wazuri kwenye ‘kufukuza mwizi’

Arsenal si wazuri kwenye ‘kufukuza mwizi’

752
0
SHARE

ARSENALLONDON, England

ARSENAL wako kwenye mbio za ubingwa msimu huu. Wanafukuzana kwa karibu na Leicester na Tottenham katika kumaliza ukame wa taji la Premier League kwa miaka 13 hivi sasa.

Bado mashabiki wa Arsenal wana imani kubwa na timu yao, lakini hii si mara ya kwanza kwa Arsenal kufukuza taji kwa mtindo huu na mwisho wa siku kuangukia pua.

Makala haya yamekuandalia orodha ya namna Arsenal alivyoweza kumaliza msimu baada ya michezo 27 ya ligi tangu msimu wa 2003-04 walipotwaa taji kwa mara ya mwisho.

2015-16

Baada ya mechi 27: Wako nafasi ya 3 na pointi 51 – pointi 5 nyuma ya vinara, Leicester City.

Mwisho wa msimu:  Tusubiri tuone.

2014-15

Baada ya mechi 27: Walikuwa nafasi ya 3 na pointi 51 – pointi 9 nyuma ya vinara Chelsea.

Mwisho wa msimu: Walimaliza nafasi ya 3 wakiwa na pointi 75 – pointi 12 nyuma ya mabingwa Chelsea.

2013-14

Baada ya mechi 27: Walikuwa kwenye nafasi ya 2 na pointi 59 – pointi moja nyuma ya vinara, Chelsea.

Mwisho wa msimu: Walimaliza nafasi ya 4, wakiwa na pointi 79 – pointi 7 nyuma ya mabingwa Manchester City.

2012-13

Baada ya mechi 27: Walikuwa kwenye nafasi ya 5, wakiwa na pointi 47 – pointi 11 nyuma ya vinara Manchester United.

Mwisho wa msimu: Walimaliza nafasi ya 4, wakiwa na pointi 73 – pointi 16 nyuma ya mabingwa Manchester United.

2011-12

Baada ya mechi 27: Walikuwa nafasi ya 4 wakiwa na pointi 49 – pointi 17 nyuma ya vinara Manchester City.

Mwisho wa msimu:  Walimaliza nafasi ya 3 wakiwa na pointi 70 – pointi 19 nyuma ya mabingwa Manchester City.

2010-11

Baada ya mechi 27: Walikuwa kwenye nafasi ya 2, wakiwa na pointi 56 – pointi nyuma ya vinara Manchester United.

Mwisho wa msimu:  Walimaliza nafasi ya 4 wakiwa na pointi 68 – pointi 12 nyuma ya mabingwa Manchester United.

2009-10

Baada ya mechi 27: Walikuwa kwenye nafasi ya 3 wakiwa na pointi 55 – pointi 6 nyuma ya vinara Chelsea.

Mwisho wa msimu:  Walimaliza kwenye nafasi ya 3, wakiwa na pointi 75 – pointi 11 nyuma ya mabingwa Chelsea.

2008-09

Baada ya mechi 27: Walikuwa kwenye nafasi ya 5, wakiwa na pointi 46 – pointi 16 nyuma ya vinara Manchester United.

Mwisho wa msimu:  Walimaliza wakiwa nafasi ya 4 wakiwa na pointi 72 – pointi 18 nyuma ya mabingwa Manchester United.

2007-08

Baada ya mechi 27: Walikuwa kwenye nafasi ya 1, wakiwa na pointi 64 – pointi 3 juu ya walioshika nafasi ya pili, Manchester United.

Mwisho wa msimu:  Walimaliza nafasi ya 3 wakiwa na pointi 83 – pointi 4 nyuma ya mabingwa Manchester United.

2006-07

Baada ya mechi 27:  Walikuwa kwenye nafasi ya 4 wakiwa na pointi 52, pointi 20 nyuma ya vinara, Manchester United.

Mwisho wa msimu:  Walimaliza nafasi ya 4, wakiwa na pointi 68 – pointi 19 nyuma ya mabingwa, Manchester United.

2005-06

Baada ya mechi 27:  Walikuwa kwenye nafasi ya 7 wakiwa na pointi 41 – pointi 28 nyuma ya vinara, Chelsea.

Mwisho wa msimu:  Walimaliza kwenye nafasi ya 4 wakiwa na pointi 67 – pointi 24 nyuma ya mabingwa Chelsea.

2004-05

Baada ya mechi 27:  Walikuwa kwenye nafasi ya 3 wakiwa na pointi 57 – pointi 11 nyuma ya vinara Chelsea.

Mwisho wa msimu:  Walimaliza wakiwa na pointi 83 – pointi 12 nyuma ya mabingwa Chelsea.

Mechi zilizosalia

Machi 2 Swansea City (Nyumbani)

Machi 5 Tottenham Hotspur (Ugenini)

Machi 12 West Bromwich Albion (Nyumbani)

Machi 19 Everton (Ugenini)

Aprili 2 Watford (Nyumbani)

Aprili 9 West Ham United (Ugenini)

Aprili 17 Crystal Palace (Nyumbani)

Aprili 24 Sunderland (Ugenini)

Aprili 30 Norwich City (Nyumbani)

Mei 7 Manchester City (Ugenini)

Mei 15 Aston Villa (Nyumbani)

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here