Home Michezo Kimataifa Arsenal yafanyiwa figisu kwa Lacazette

Arsenal yafanyiwa figisu kwa Lacazette

474
0
SHARE
Alexandre Lacazette

LONDON, England

KLABU ya Lyon imethibitisha kuwa imeipiga chini ofa ya pauni milioni 29 iliyowekwa mezani na Arsenal kwa ajili ya straika wao, Alexandre Lacazette.

Kupitia mtandao wa Twitter, Lyon walifafanua vyema kuhusu suala la Lacazette na kusisitiza kuwa hawako tayari kumuuza kwa kuwa bado hawajapata mrithi wake.

Mapema wiki hii gazeti la Le Progres, la nchini Ufaransa liliripoti kuwa ofa ya Arsenal iliyokataliwa ni pauni milioni 40.2 jambo ambalo limepingwa vikali na Lyon.

“Olympique Lyon tunakanusha taarifa zilizoandikwa na gazeti la Le Progres kuwa tumepokea ofa ya pauni milioni 40 kutoka kwa Arsenal kwa ajili ya Alexandre.

“Kama klabu tunasikitishwa na taarifa hizi na tunawaomba wahusika wa Le Progres wawe wanawasiliana na sisi kwanza kabla ya kuandika habari zao.

“Ukweli ni kuwa, klabu ya Arsenal ilituma kweli ofa ya pauni milioni 35 na Lyon tulikataa kwa sababu moja tu. Hatujapata mbadala wa Lacazette mpaka sasa katika kikosi chetu.”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here