SHARE

LONDON, England

BAADA ya kushinda michezo miwili mfululizo, Arsenal walijikuta waking’ang’anizwa sare ya bao 1-1 na wenyeji wao Crystal Palace katika Uwanja wa Selhurst Park.

Dakika ya 12, Arsenal walitangulia kuziona nyavu za wapinzani wao kwa bao lililofungwa na straika wao Pierre Emerick-Aubameyang huku Crystal Palace walisawazisha dakika ya 54 kupitia kwa Jordan Ayew.

Hata hivyo, Aubameyang alishindwa kumaliza mechi hiyo baada ya kuoneshwa kadi nyekundu dakika ya 67 kwa kumchezea rafu mbaya kiungo Max Meyer.

Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta aliamini sare hiyo imetokea kama bahati, kwani kabla ya kadi nyekundu walikuwa wakiumiliki mchezo huo.

“Hatukucheza vibaya, lakini hatukuwa na bahati, ukitazama tulimiliki mchezo kwa kiasi kikubwa kabla ya kadi nyekundu,” alisema.

Baada ya sare hiyo, Arsenal wanasalia nafasi ya 10 katika msimamo wa Ligi Kuu England wakiwa na pointi 28 huku wapinzani wao wakiwa juu yao kwa tofauti ya pointi moja tu. 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here