SHARE

MILAN, Italia

WANACHOSIKILIZIA mabosi wa Inter Milan ni hatima ya mshambuliaji wao, Lautaro Martinez, kwamba kama Barcelona watamchukua, basi wao washushe majembe hayo ya Ligi Kuu ya England.

Martinez ameshapachika mabao 16 katika mechi 31, hivyo viongozi wa Barca wanamuona nyota huyo kuwa ndiye mrithi sahihi wa Muargentina mwenzake, Lionel Messi.

Inter chini ya kocha Antonio Conte, nao wameshajipanga kuishi bila yeye, na ni Pierre-Emerick Aubameyang na Olivier Giroud ndiyo wanaoonekana kuweza kuziba pengo lake.

Aubameyang, ambaye amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake na Arsenal, alitakiwa Inter Januari, mwaka huu, lakini dili lilikwama kwa kuwa Washika Bunduki hawakuwa tayari kumwachia.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here