SHARE

NA JESSCA NANGAWE

BAADA ya kuwepo sintofahamu ya ukaribu wa mastaa wawili Aunt Ezekiel na Wema Sepetu, hatimaye majibu yamepatikana.

Akizungumza na DIMBA Jumatano, staa wa Bongofleva Aunt Ezekiel amekiri kuwa ukaribu wake na rafiki yake huyo umepungua kutokana na kubanwa na majukumu pamoja na kipindi hiki dunia kupambana na janga la Corona.

Aunt alisema, kutokana na hali halisi ya maisha kila mmoja amekua bize na shughuli zake lakini haimaanishi hawapo pamoja.

“Unajua maisha ya sasa yamebadilka,si rahisi mtu ukapata muda wa kukaa na watu.kwanza sahivi kila mtu anatakiwa akae kwake..huu ugonjwa ni hatari sana..lazima tukimbizane na maisha,na ndio kinachotokea kati yangu na Wema’ Alisema Aunt.

Aidha Aunty amekiri kupindi hiki ameamua kujitenga zaidi yeye na familia yake hasa kutokana na janga hili la corona.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here