SHARE

NA BRIGHITER MASAKI (TSJ)

MUDA mfupi baada ya wasanii wa Tanzania kutwaa tuzo mbalimbali za Eatv, baadhi ya wanamuziki wenzao wamejitokeza hadharani kuelezea mapungufu kadhaa yaliyojitokeza katika uandaaji.

Miungoni mwao ni msanii mkongwe Ambwene Yesaya maarufu kama AY ambaye alindika katika mitandao ya kijamii akidai kwamba binafsi haoni kama kuna usawa katika hafla nzima ya ugawaji tuzo katika nchi hii.

Alitoa mfano juu ya kosa kubwa la kushirikishwa mashabiki kwa asilimia 100 bila kuwepo majaji, kwamba kunaweza kusababisha maamuzi yasiyo ya haki yakatokea.

“Ilitakiwa angalau kuwe na asilimia 30 ya majaji ambao wangeratibu na kisha kutoa maamuzi ya kitaalamu kuhusu ushindi wa muhusika” alisema.

Kwa upande mwingine msanii maarufu wa Bongofleva, Mwana FA, yeye alisema kama yeye angeshirikishwa kuchagua msanii wa mwaka asingesita kumtaja Ali Kiba na Darasa ambao anasema kazi zao ziko wazi na zinaonekana bila kupepesa macho.

Pia ameutaja wimbo bora kwake kuwa ni Aje na mwingine ni Muziki.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here