SHARE

NA WINFRIDA MTOI


TIMU ya Azam leo inashuka dimbani kuvaana na JKT Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, utakaopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, jijini Dar es Salaam.


Mchezo huo utakuwa wa 10 kwa Azam ambayo imetoka kupata ushindi mnono baada ya kuichapa Alliance FC mabao 5-0 mechi iliyopigwa Jumanne iliyopita, Uwanja wa Nyamagana, Mwanza.
JKT Tanzania inakutana na Azam ikiwa imetoka kushinda mechi iliyopita kwa mabao 2-1 dhidi ya Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Dar es Salaam.

Katika msimamo wa ligi hiyo, Azam inashika nafasi ya nne na pointi 19, ikishuka dimbani mara tisa, imeshinda sita, imetoa sare moja na kupoteza mbili.


Maafande wa JKT wamecheza mechi 11, wameshinda nne, sare tatu na kupoteza nne, hivyo kujikusanyia pointi 15 na kukaa nafasi ya 13.
Wakizungumzia mchezo huo kocha Msaidizi wa Azam, Idd Nassor ‘Cheche’, alisema wamefanya mazoezi tangu waliporejea kutoka Mwanza ili kurekebisha baadhi ya makosa.


Kwa upande wake Kocha Mkuu wa JKT Tanzania, Abdallah Mohammed ‘Bares’, alisema mchezo utakuwa mgumu kutokana na ubora wa kikosi cha Azam, lakini anaamini hata nyota wake wako vizuri.
@@@@@

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here