Home Habari Azam kunogesha Ndondo Cup

Azam kunogesha Ndondo Cup

300
0
SHARE

NA TIMA SIKILO

KITUO cha bidhaa za Azam kilichopo Magomeni, Dar es Salaam kimetangaza kuwa mmoja wa wadhamini wa michuano ya Ndondo Cup iliyopo chini ya Clouds Media Group.

Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano, Shaffih Dauda, aliliambia DIMBA Jumatano kuwa Magomeni Ice Cream Center watakuwa sehemu ya wadhamini wa michuano kwa kutoa ofa ya kinywaji kwa kila shabiki atakayeingia uwanjani katika sherehe za ufunguzi za Ndondo Cup hatua ya 32 bora.

“Juni 7 utachezwa mchezo wa kwanza wa ufunguzi wa michuano ya Ndondo Cup hatua ya 32 bora kati ya Keko Furniture na Toroli Combine, kiingilio ni Shilingi 2,000 na shabiki ataingia uwanjani na kupewa ofa ya kinywaji kimoja kutoka kituo cha Ice Cream cha Azam kilichopo Magomeni,” alisema Shaffih.

Naye Meneja wa kituo hicho, Ibrahim Wasome, amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanjani huku akisisitiza kuwa wauzaji wa bidhaa zao watakuwepo katika Uwanja wa Bandari na kuuza bidhaa kwa bei rahisi (jumla) tofauti na ilivyozoeleka.

“Hii ni fursa hata kwa wafanyabiashara kujitokeza na kununua bidhaa zetu kwa wingi,” alisema Wasome.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here