Home Habari AZAM: MTAPATA TABU SANA KWA NGOMA

AZAM: MTAPATA TABU SANA KWA NGOMA

7213
0
SHARE
NA SAADA SALIM          |  

UONGOZI wa Azam FC umeweka bayana kuwa straika wao mpya, Donald Ngoma, atawasumbua sana mabeki wa timu pinzani msimu ujao kwani afya yake inazidi kutengemaa.

Ngoma ambaye alikuwa mwiba mkali na kikosi cha Yanga, alijikuta akikaa nje ya uwanja kwa muda mrefu kutokana na majeraha yaliyokuwa yakimsumbua, lakini Azam wakamsajili na kumpeleka Afrika Kusini kupata matibabu zaidi.

Ilibidi Yanga wavunje mkataba na Ngoma walipoona hatumiki na walivyofanya hivyo tu, Azam FC wakamsajili na sasa wanadai kuwa shughuli yake msimu ujao wapinzani wataomba poo.

Akizungumza na DIMBA Jumatano, Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Azam, Idrissa Nassor ‘Father’, alisema Ngoma ni mtu sahihi wa kuziba pengo la nahodha wao wa zamani, John Bocco ambaye kwa sasa anauwasha moto akiwa Simba.

“Ngoma ni mbadala sahihi wa Bocco, tayari ameshapewa matibabu na daktari kutoa taarifa ya kina kuwa kuanzia  Agosti 11, mwaka huu, straika huyo kutoka Zimbabwe atakuwa fiti kuiwakilisha timu yao katika mashindano mbalimbali,” alisema.

Baada ya kumchukua kutoka Yanga, walimpeleka katika Hospitali ya Vincent Pallotti jijini Cape Town, Afrika Kusini kupata vipimo zaidi na kukutwa na tatizo la kuchanika mtulinga wa mbele wa goti la mguu wa kulia (Anterior Cruciate Ligament).

Daktari Mkuu wa timu hiyo, Mwanandi Mwankemwa aliyeongozana na Ngoma jijini humo, alisema baada ya uchunguzi madaktari hao waliangalia mtulinga huo (ligament) na kubaini kuwa umeanza kupona na ataweza kurejea kwenye ushindani mapema iwezekanavyo.

“Bahati yake hatafanyiwa upasuaji, atatakiwa kufanya mazoezi ya kawaida yasiyohusisha kulipa tabu goti lake (yatakayolishtua goti), kwa namna yoyote ile, katika wiki tatu hizi za kwanza kuanzia akiwa kwao Zimbabwe.

“Atakaporudi hapa baada ya wiki tatu kupita kuanzia sasa, Ngoma atakuwa Chamazi (Azam Complex), akienda kwenye kliniki ya London Health Centre kuendelea na programu na kuanza kukimbia kwa kasi na ataruhusiwa kurejea uwanjani kwa mechi za ushindani kuanzia Agosti 11, mwaka huu,” alisema Mwankemwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here