SHARE

JESSCA NANGAWE NA NYEMO MALECELA

AZAM imeendelea kujiweka sawa na mbio ubingwa wa Ligi Kuu Bara

baada ya jana kuitandika Polisi Tanzania bao 1-0, mchezo uliopigwa uwanja wa Uhuru, jijini Dar es salaam.

Bao pekee la Azam liliwekwa wavuni na Mudathir Yahya, dakika 48 na kuifanya timu hiyo kufikisha alama 44 huku ikiendelea kubaki nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi hiyo huku Simba wakiwa bado vinara.

Mara baada ya mchezo huo Kocha Mkuu wa Azam, Aristica Cioaba alikiri kuwa ana kazi kubwa ya kuhakikisha vijana wake wanaendeela kupambana ili kujitengenezea mazingira mazuri zaidi kwa kuwa safari ya kuwania ubingwa bado ndefu.

“Tumeshinda, lakini kikubwa vijana wanapaswa kupambana, kazi ni kubwa mbele kama tuinahitaji kupata ubingwa ama kuwa nafasi tatu za juu”alisema Cioaba.

Katika mchezo mwingine Namungo ya Lindi nayo imesogea hadi nafasi

ya nne 36 baada ya jana kuitandika Singida United bao 1-0 ikiwa kwenye uwanja wake wa nyumbani wa Majaliwa.

Nao Kagera wamejikuta wakibanwa mbavu katika uwanja wao wa nyumbani wa Kaitaba baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-1 mbele ya Alliance katika mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Kaitaba, Mkoani Kagera.

Huu unakua mchezo wa pili kwa Kagera kushindwa kutumia nafasi yake vyema baada ya mchezo uliopita kukubali sare ya 0-0 mbele ya Biashara United.

Biashara nao walitumia vyema nafasi yao kwa kuichapa Mbao bao 1-0 huku Lipuli na JKT Tanzania zikitoshana nguvu kwa kutoka sare ya 1-1 Kwenye uwanja wa Samora, Iringa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here