SHARE

NA TIMA SIKILO, KIGALI

KOCHA Mkuu wa timu ya Azam FC, Etiene Ndayiragije ameahidi kurudi na kombe la michuano ya CECAFA, KAGAME CUP 2019 nchini Tanzania.

Azam FC ndio Mabingwa watetezi wa michuano hiyo kwa msimu wa 2018 na leo wanatarajiwa kucheza fainali dhidi ya timu ya KCCA ya nchini Uganda.

Katika mchezo wao wa kwanza hatua ya Makundi uliochezwa kwenye Uwanja wa Huye nchini Rwanda KCC walifanikiwa kuwafunga Azam FC bao 1-0.

Hata hivyo Azam jana walifinikiwa kutinga fainali baada ya kuwatoa Maniema FC katika nusu fainali iliyochezwa juzi kwenye Uwanja wa Kigali kwa mikwaju ya Penati 4-5.

Akizungumza na DIMBA jana, Ndaiyaragije alisema anashukuru kutinga nusu fainali na furaha yake ni kuona anarudi na kombe hilo nyumbani.
Naye Straika wa timu hiyo Mzimbabwe Donald Ngoma, amesema ubingwa wa CECAFA KAGAME CUP 2019 ni lazima watarudi nao nyumbani.

Azam leo wanatarajiwa kucheza fainali ya michuano hiyo dhidi ya KCCA ya Uganda katika Uwanja wa Kigali, baada ya kufanikiwa kuwatoa Maniema FC, ya nchini DR Congo kwa mikwaju ya Penati 4-3.

Akizungumza na DIMBA baada ya mchezo wao Ngoma alisema wamefurahi kutinga nusu fainali na kwa sasa wanachoangalia zaidi ni fainali.

Alisema anaamini wananafasi ya kutetea ubingwa wao huo kutokana na jinsi wanavyozidi kukua kiwango katika kila mchezo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here