SHARE

NA JESSCA NANGAWE

UONGOZI wa klabu ya Azam FC umesema utakuwa bega kwa bega na familia ya nahodha wao, Aggrey Morris, aliyefiwa na mkewe akiwa kwenye harakati za kujifungua.

Aggrey aliondokewa na mkewe aitwaye Asteria juzi usiku akiwa hospitalini alipokua amekwenda kwa ajili ya kujifungua.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, Abdul Amin Popat, alisema wamepokea kwa masikitiko makubwa msiba huo mzito kwa familia ya Aggrey na watakuwa bega kwa bega na familia ya mchezji huyo katika kipindi hiki kigumu.

“Tunatoa salamu zetu za pole kwenda kwa familia ya Morris pamoja na ndugu, jamaa na marafiki na wote walioguswa na msiba huo, Azam FC tunaungana na familia ya marehemu na tunamuomba Mwenyezi Mungu awajalie nguvu na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu,” alisema Popat.

Aidha alisema baada ya kuwasiliana na uongozi wa familia ya Agrey mazishi yanatarajia kufanyika katika makaburi ya Nyantila yaliyopo Kitunda jijini Dar es Salaam kesho.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here