SHARE

NA MARTIN  MAZUGWA


MABINGWA wa kombe la Klabu Bingwa Afika Mashariki na Kati, Azam FC, wapo kwenye mchakato wa kutafuta kocha mpya ambaye ataziba nafasi ya kocha  Mhispania, Zeben Hernandez, aliyetupiwa virago baada ya timu kupata matokeo yasiyoridhisha.

Zeben amefukuzwa mara baada ya kuiongoza timu hiyo katika michezo 18, akishinda mechi nane, sare sita na amepoteza nne, lakini akawapatia matajiri hao Ngao ya Hisani mara baada ya kuifunga Yanga kwa mikwaju ya penalti.

Azam, ambao msimu uliopita walishika nafasi ya pili katika katika msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, msimu huu hali imekuwa tofauti, ambapo wanakamata nafasi ya tatu wakiwa na pointi 30, sawa na Mtibwa Sugar wanaoshika nafasi ya nne, wakitofautiana kwa idadi ya mabao ya kufunga na kufungwa.

Makocha ambao wanatolewa macho na matajiri hao ni pamoja na Lamine Nd’iye, raia wa Senegal ambaye aliipa taji la klabu bingwa Afrika klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, Zdravko Logarusic aliyewahi kuinoa Simba na FC Leopard ya nchini Kenya.

Habari nyingine zinadai kuwa, Wanalambalamba hao wanataka kumrudisha nchini aliyewahi kuwa kocha mkuu wa klabu ya Yanga  anayeifundisha timu ya Taifa ya Uganda, Milutin Sredojević,  ambaye ana uzoefu na soka la Afrika.

Makocha hao licha ya kuwa na vyeti vizuri, lakini pia wana uzoefu na soka la Afrika ambalo lina changamoto nyingi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here