Home Dondoo za Ulaya Balotelli amshawishi Sakho atimke Liverpool

Balotelli amshawishi Sakho atimke Liverpool

454
0
SHARE
Mamadou Sakho

MSHAMBULIAJI wa zamani wa klabu ya Liverpool anayekipiga Nice ya Ufaransa, Mario Balotelli, amemtaka beki wa Liverpool, Mamadou Sakho, kuondoka kwenye viunga vya Anfield mara tu dirisha dogo la usajili litakapofunguliwa Januari, mwakani.

Sakho hajatumika kwenye kikosi cha kwanza cha Liverpool msimu huu chini ya kocha Jurgen Klopp, tangu aliporudishwa jijini Merseyside wakati timu hiyo ilipokuwa kwenye maandalizi ya msimu nchini Marekani.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here