Home Habari BANDA AMPANIA STRAIKA LIGI KUU ENGLAND

BANDA AMPANIA STRAIKA LIGI KUU ENGLAND

6346
0
SHARE

NA MAREGES NYAMAKA

BEKI wa kati wa timu ya Taifa, Taifa Stars, Abdi Banda, amesema atahakikisha anatimiza majukumu yake ya kumdhibiti straika wa timu ya Taifa ya Algeria anayekipiga katika klabu ya Leicester City ya England, Riyad Mahrez.

Mahrez ambaye ni mwanasoka bora wa Afrika msimu uliopita, ni miongoni mwa wachezaji wa timu ya taifa ya Algeria wanaotarajia kushuka dimbani keshokutwa kuwavaa Stars iliyo chini ya kocha Salum Mayanga.

Akizungumza na DIMBA Jumatano, Banda aliweka wazi kuwa anauchukulia mchezo kwa ukubwa wake, lengo likiwa ni kupata matokeo bora ambayo huenda yakaifanya  Stars kupanda viwango vya ubora vya Fifa.

“Tunacheza na timu kubwa yenye umahiri kila eneo la uwanja, ukizingatia wachezaji wake asilimia kubwa wanacheza timu mbalimbali kubwa ikiwamo barani Ulaya, cha kwanza ni kutimiza majukumu yangu na kutowapa nafasi washambuliaji,” alisema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here