SHARE
Clatous Chama

NA WINFRIDA MTOI

KITENDO cha kiungo wa Simba, Clatous Chama, kuwafunga Nkana na kuwatoa matika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, bado tukio hilo loinamtesa kwa mashabiki nchini Zambia aliko hivi sasa.

Hali hiyo inamfanya  mchezaji huyo aonekane hana uzalendo, hivyo baadhi ya mashabiki wa Nkana kuonekana kuchukizwa na tukio lile bila kujali kwamba amekuwa akitekelea majukumu yake.

Chama ambaye ni raia wa Zambia, timu hiyo ilipo, mashabiki wake wamekuwa wakimnanga katika mitandao yake ya kijamii baada ya kuweka video ya kuzungumzia bao hilo.

Pamoja na wapenzi wengi wa soka kumuunga mkono, mashabiki wa Nkana, wanamueleza wazi kuwa kitendo cha kutaja bao hilo, inatokana na Chama kuichukia timu hiyo kwa sababu aliwahi kuichezea katika ligi ya Zambia.

Hivi karibuni Chama aliweka video katika instagram na kutaja mabao yake matatu makali,  yakiwamo aliloifunga  Sevilla ya Hispania, mwaka jana katika mchezo wa kirafiki  waliofungwa 5-4, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Lingine ni aliloifunga AS Vita, katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, wakati Simba ilipopata ushindi wa 2-1, Uwanja wa Taifa na kutinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here