SHARE

NA RAMADHAN HASSAN, DODOMA

MARA baada ya kumalizika kwa Ligi Kuu ya Soka ya Wanawake, Kocha Mkuu wa timu ya Baobab Queens ya jijini hapa, Musa Furtune, amewauma sikio viongozi wa timu hiyo kwa kuwataka msimu ujao kusajili kikosi kipana.

Baobab Queens imemaliza ligi hiyo kwa kujikusanyia pointi 21 ikishika nafasi ya 8, huku JKT Queens ikiibuka bingwa wa ligi hiyo kwa kujikusanyia pointi 66.

Akizungumza na DIMBA Jumatano juzi jijini hapa, Furtune alisema licha ya kikosi chake kucheza kwa kujituma lakini kilikuwa na mapungufu kutokana na kuwa na wachezaji wachache.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here