Home Burudani BARAKA DA PRINCE, JUX, BEN POL WAMKUNA CHRISTIAN BELLA

BARAKA DA PRINCE, JUX, BEN POL WAMKUNA CHRISTIAN BELLA

469
0
SHARE

NA JESSCA NANGAWE,

MKALI wa Masauti ndani ya muziki wa dansi nchini, Christian Bella, amesema ushirikiano unaofanywa na nyota watatu wa muziki wa kizazi kipya, Juma Jux, Baraka Da Prince na Ben Pol unaweza kuipaisha Tanzania katika ramani kimataifa.

Bella ameliambia DIMBA Jumatano kwamba, wasanii hao wana nafasi kubwa ya kuuweka muziki huo kwenye ramani bora kimataifa kwa namna walivyoamua kutoka kivingine na tayari wameongeza ushindani kwa Diamond Platnum na Ali Kiba.

Aliwasifu kwa namna ambavyo wamekuwa wakifanya kazi bora kwenye muziki huo na kujitofautisha na baadhi ya wasanii waliowakuta kwenye gemu, hivyo kujizolea umaarufu kila kukicha.

“Hawa madogo napenda sana jitihada zao, wamekuwa wakifanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na pia kazi zao zinaonekana sana, wanajitahidi na naamini watafika mbali zaidi ya hapa walipo,” alisema Bella.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here