SHARE

NA JESSCA NANGAWE

BAADA ya kuondoka kwenye lebo ya Rockstar 4000, msanii wa Bongo Fleva, Baraka Da Prince, alidaiwa kupotea kimuziki, lakini mwenyewe amefunguka na kusisitiza yupo kwenye kiwango chake na kamwe hawezi kuchuja kirahisi.

Tangu msanii huyo aondoke katika lebo ya RockStar4000, kumekuwa na taarifa zinazodai msanii huyo ameyumba kiuchumi hadi kupelekea kuuza baadhi ya mali zake kitu ambacho amekikanusha.

“Watu wanajaribu kutengeneza stori kwa ajili ya kuniharibia lakini hilo halitawezekana, kwa kuwa najiamini na ninafanya kazi nzuri kupitia muziki wangu,” alisema Barakah.

Barakah kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ya ‘Sometime’ ikiwa ni ya pili kutoka chini ya lebo yake  mpya ya‘Bana Music’, baada ya ile ya mwanzo ambayo ilikuwa ya Naj iliyojulikana kama ‘Utanielewa’.

&&&&

Aunty Ezekiel ajikita kwenye ujasiriamali

NA JESSCA NANGAWE

STAA wa Bongo Movies, Aunt Ezekiel, amesema pamoja na sanaa yake ya kuigiza lakini amekuwa akijishughulisha zaidi na ujasiriamali kwa lengo la kujiongezea kipato.

Akizungumza na DIMBA Jumatano, Aunt amesema ameamua zaidi kuwekeza kwenye biashara kwa kuwa kutegemea uigizaji hakumlipi kulingana na jinsi soko lake lilivyo na maisha ya sasa.

“Unajua bado kwa hapa kwetu huwezi kusema unategemea uigizaji ili uishi mjini, Bongo Movie hailipi, nahitaji kupanua mawazo na kufanya mambo mengine ambayo yataniongezea kipato, kwa sasa nafanya biashara zangu ambazo kwa kiasi kikubwa zinaniongezea kipato,” alisema Aunt.

Aunt ambaye ni mzazi mwenzake na mnenguaji kutoka WCB, Mose Iyobo, ameongeza kuwa mbali na biashara yake ya kuuza sabuni na kusambaza katika mikoa mbalimbali, pia amekuwa akijishughulisha na kutangaza bidhaa mbalimbali huku akiwataka wanawake wenzake kutojisahau na kutegemea kusaidiwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here