Home Habari Baraza la Wazee Yanga Sc wapinga kukodishwa kwa klabu yao

Baraza la Wazee Yanga Sc wapinga kukodishwa kwa klabu yao

635
0
SHARE

KATIBU mkuu wa Baraza la Wazee wa klabu ya Yanga, Ibrahim Akilimali pamoja na wenzake, wamepinga suala la klabu yao kuingia makubaliano na Kampuni ya Yanga yetu kwa ajili ya kukodisha klabu hiyo kwa miaka 10.

Wakizungumza na waandishi wa Habari jana kwenye Ukumbi wa  Habari Maelezo, Akilimali alisema, mkataba huyo uliosainiwa na lilalotajwa kuwa ni baraza la wadhamini ni batili na wala hawaitambui kwani kwa kufanya hivyo wanaweza kusababisha kuigawa timu hiyo kwenye makundi jambo ambalo hawakubaliani nalo.

“Huko nyuma kuliwahi kutokea mgogoro mkubwa kwenye klabu yetu kutokana na masuala ya Kampuni na kujikuta tukigawanyika kwenye makundi matatu, jambo hilo tulilishughulikia na kuisha hivyo  tuliapa kutoruhusu mvuruganio tena kwenye klabu yetu, na hili suala la kukodishwa hatukubaliani nalo kwani YAnga haiwezi kukodisha kama masufulia ya shughulini,” alisema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here