SHARE

CARALUNYA, Hispania

MTANANGE wa marudiano kuisaka robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kati ya Barcelona na Napoli utachezwa bila mashabiki kutokana na hofu ya maambukizi ya virusi vya Corona.

Mechi hiyo ya pili itachezwa Jumatano ya wiki ijayo katika Uwanja wa Camp Nou, ikumbukwa kuwa ile ya kwanza kule Italia ilimalizika kwa sare ya bao 1-1.

Tahadhari ya mabosi wa Barca inatokana na ukweli kwamba Italia inatajwa kuwa na maambukizi ya virusi hivyo, ikifikia hatua ya baadhi ya mechi kupigwa kalenda, huku zingine zikichezwa bila mashabiki.

Katika mechi ya kwanza, Napoli walitangulia kwa bao la Dries Mertens, kabla ya Antoine Griezmann kuisawazishia Barca.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here