Home Michezo Kimataifa Barca wanarudi tena kuibomoa Arsenal

Barca wanarudi tena kuibomoa Arsenal

478
1
SHARE

BARCELONA, Hispania

HATIMAYE klabu ya FC Barcelona imethibitisha kuwa itamsajili beki wa kulia wa Arsenal, Hector Bellerin, wakati wa dirisha dogo la usajili, Januari mwakani.

Taarifa hii imetoka baada ya kuwepo kwa tetesi kuwa Barca ndio walikuwa wakimshawishi Bellerin asiongeze mkataba mpya na washika mitutu wa jiji la London.

Akizunguza na jarida la SPORT, Makamu wa Rais wa Barca, Jordi Mestre, alisema kuwa wamedhamiria kumrejesha Bellerin, aliyeondoka kwenye kituo chao cha La Masia akiwa na miaka 16
“Iko wazi, ni mpango wetu kwenye dirisha dogo la usajili. Ni mchezaji mkubwa na tutahahakikisha anarudi nyumbani,” alisema Mestre.

“Wenger alifanikia kumshawishi kuondoka hapa mwaka 2011, akimuahidi kumpatia mkataba, jambo ambalo lilikuwa gumu kwetu.
“Isingewezekana kumuahidi kuwa angecheza kwenye kikosi cha kwanza huku tukiwa na Dani Alves kwenye nafasi yake.”
Hii si mara ya kwanza kwa Barca kuwasajili makinda waliowalelea kwenye kituo chao cha soka, hali inayomfanya Mestre kuamini hakutakuwa na ugumu wowote kwa Bellerin.

“Ni jambo zuri kuona wakiondoka na kwenda kupata uzoefu kisha wakarejea wakiwa bora,” aliongeza makamu huyo.
“Watazame kina Cesc Fabregas, Gerard Pique, Jordi Alba na Denis Suarez… na tuna imani itakuwa vyema pia kwa kijana wetu, Sergi Samper.

Mkataba wa Hector Bellerín na Arsenal unamalizika mwaka 2019, lakini bado Arsene Wenger amekuwa kwenye mipango ya kumshawishi kinda huyu kubaki London mpaka mwaka 2021.
Mpaka sasa thamani ya Bellerin ni pauni mil 40 na endapo dili hili likifanikiwa, atafanikiwa kuwa beki ghali zaidi duniani.

1 COMMENT

  1. Tunachoangalia. sisi ni ushindi. bila kujali. ni nani amepangwa. ,kwa. sasa. wenye kusema. wazidi tu. kusema. kwani. hawana. tofauti. sana. na. mabingwa. wa. mdomo ktk kusema. nchini. mwetu. Tanga. Nao. majibu. yao hayako. mbali. sana. (Oktoba). modi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here