Home Michezo Kimataifa BARCELONA YAMUUMIZA KICHWA SIMEONE

BARCELONA YAMUUMIZA KICHWA SIMEONE

615
0
SHARE
Diego Simeone

MADRID, Hispania

MSIMU huu umekuwa mgumu kwa Atletico Madrid ambapo hadi kufikia sasa wanakamata nafasi ya nne nyuma ya vinara Barcelona, Real Madrid na Sevilla huku wakikabiliwa na mchezo mgumu wa nusu fainali ya Copa del Rey dhidi ya Barcelona.

Atletico wameonja ushindi mara moja tu dhidi ya Barca katika jumla ya michezo sita ya mwisho waliyokutana, huku ushindi huo ukiwa ni kwenye hatua ya mtoano Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka jana.

Lakini kocha Diego Simione, kwa upande wake anaonekana kutokuwa na wasiwasi juu ya mtanange huo akisema kuwa ili kunyakua mataji ni lazima uzifunge timu kubwa.

Kauli yake hiyo inaonekana kukinzana na takwimu zake dhidi ya Barca na Madrid msimu huu ambapo kwenye mechi mbili za La Liga ameambulia pointi moja tu dhidi yao (sare ya 1-1 kwa Barca, kichapo cha bao 3-0 kwa Madrid).

Kwa hali yoyote ile, Simione ana mtihani mzito wa kuidondosha Barca ili anyakue angalau taji moja msimu huu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here