Home Burudani BARNABA KUWASINDIKIZA MAMISS

BARNABA KUWASINDIKIZA MAMISS

6285
0
SHARE

NA JESSCA NANGAWE


MKALI wa muziki wa Bongo Fleva, Barnaba Boy, wikiendi hii atauhanikiza usiku wa maraha kwa kupiga shoo ya kukata na mundu ndani ya Ukumbi wa Mfipa Lounge uliopo Mwanagati jijini Dar, katika onyesho maalumu la kuwasindikiza washiriki wa shindano la Miss Ambassador Mfipa.

Msemaji wa onyesho hilo, Emmanuel Lazaro, alisema Barnaba ataongozana na madansa wake ambao wameahidi kuonesha umahiri mkubwa wa kucheza staili mbalimbali za muziki.

Lazaro alisema ili kumshuhudia Barnaba na madansa wake wakitimbwirika na mamiss, hakutakuwa na kiingilio zaidi ya kununua kinywaji tu kabla ya baadaye kujimwaga na disko chini ya ma-dj mahiri.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here