Home Habari BECKHAM AKATAA KULA NYOKA CHINA

BECKHAM AKATAA KULA NYOKA CHINA

870
0
SHARE

LONDON, England

DUNIA hii ina mambo na wanakwambia tembea uone ili ujifunze na kuelewa dunia inakwendaje na ina watu wa aina gani.

Lakini unapofikiria kuwa kwako kuna vituko au maajabu basi inawezekana si hivyo ila kwa wenzako ndiyo yapo maajabu makubwa na ya kushangaza.

Ulishawahi kusikia au kuambiwa kwamba nyoka ambaye kwa Tanzania na mataifa mengine ni adui mkubwa wa mwanadamu huwa analiwa kama ilivyo aina nyingine ya vitoweo?

Iko hivi, dunia ya sasa kuna maajabu ambayo watu wamekuwa wakisikia au kuyaona kwenye picha na video mbalimbali kutokana na kukua kwa teknolojia ya bahari na mawasiliano.

Miongoni mwa watu waliokutana na maajabu hayo ni Nahodha wa zamani wa England na mchezaji wa klabu za Manchester United ya England na Real Madrid ya Hispania, Devid Beckam, baada ya kukataa kula chakula kilichoandaliwa kwa kutumia kitoweo cha nyoka.

Nyota huyo aliliambia jarida moja nchini England kwamba, mwaka jana alipokuwa kwenye matembezi yake nchini China, alikataa chakula hicho ambacho kilikuwa kimeandaliwa na wenyeji wake kwa heshima, hivyo kuomba kupewa aina nyingine ya chakula.

“Mwaka jana kwenye mapumziko yangu nilikataa kula nyama inayotokana na nyoka. Nilijitahidi kufanya hivyo lakini ilishindikana hivyo nikawaambia waniandalie aina nyingine ya chakula.

“Japo nyota hao walikuwa wameandaliwa vizuri na walikuwa wakivutia sana, lakini binafsi wala familia yangu hakuna aliyekuwa tayari kula chakula hicho ambacho kwetu ilikuwa ni cha ajabu na cha kushangaza.

“Nilikuwa naambiwa na kusoma tu kwamba, nyoka ni kitoweo katika baadhi ya mataifa lakini nilikuja kujua ukweli huo hadharani baada ya kuona minofu ya nyoka,” alisema nyota huyo wa zamani wa klabu ya LA Galaxy ya Marekani.

Kwa muda mrefu China imekuwa ikitajwa kuwa ni sehemu ambapo nyoka wanaliwa kama ilivyo vitoweo vya aina nyingine.

Mbali na China lakini mataifa mengine ambayo yanatajwa kupenda kitoweo hicho ambacho kwa nchi za Kiafrika hakiliwi, ni pamoja na Indonesia, Burma na Thailand nchi ambazo pia zipo jirani lakini zikiwa na utamaduni unaofanana kwa kiasi kikubwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here