Home Habari Bei ya mafuta yazuia PSG kuivaa Montpellier

Bei ya mafuta yazuia PSG kuivaa Montpellier

3876
0
SHARE

PARIS, Ufaransa

IFAHAMIKE kuwa jijini Paris kuna maandamano ya wananchi wanaopinga ongezeko la bei ya mafuta, hali ambayo imesababisha kusogezwa mbele kwa mchezo kati ya PSG na Montpellier.

Polisi ndio walioomba mtanange huo wa Ligi Kuu ‘Ligue 1’ usichezwe Jumamosi ya wiki hii na badala yake utafutiwe siku nyingine.

Katika maandamano hayo yaliyowalazimu polisi kutumia mabomu ya machozi, watu watatu wamesharipotiwa kupoteza maisha.

PSG watashuka dimbani baada ya sare ya mabao 2-2 katika mchezo uliopita dhidi ya Bordeaux, ambapo matokeo hayo yaliwazuia kushinda mechi yao ya 14 mfululizo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here