Home Michezo Kimataifa BEKI MPYA UNITED ANASUBIRI KUTANGAZWA TU

BEKI MPYA UNITED ANASUBIRI KUTANGAZWA TU

617
0
SHARE
Victor Lindelof

LISBON, Ureno

BEKI Victor Lindelof ni kama amethibitisha kuwa ameshamalizana na Manchester United na kinachosubiriwa ni dirisha la usajili lifunguliwe ili aweze kutangazwa.

Lindelof anayekipiga katika klabu ya Benfica ya Ureno, alibambwa akisaini jezi ya Manchester United aliyopewa na shabiki mmoja wa United aliyekutana naye njiani.

Shabiki huyo aliyefahamika kwa jina la Martin Liss, alimsimamisha Lindelof na kumwomba amsainie jezi hiyo na beki huyo hakuwa na kinyongo akaisaini.

“Alicheka na alikuwa mwenye furaha sana, nafikiri anaipenda Manchester United,” alisema shabiki huyo alipohojiwa na waandishi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here